.

.

Alshabaab washukiwa kuteka nyara raia

ZePLAN | 08:00:00 | 0 comments

 

   
                                   
Wanamgambo wanaoaminika kuwa Al Shabaab wamemteka nyara chifu na gari la miraa katika eneo la Arabia, kaunti ya Mandera.
Shambulizi hilo limetokea mapema siku ya Alhamisi , na maafisa wa usalama wako katika harakati ya kuwaokoa manusura waliotekwa nyara.
Viongozi wamesema washambuliaji walionekana kufahamu eneo hilo na pia Chifu waliyemteka nyara. Inasemekana kuwa Chifu huyo alikuwa akielekea Mandera wakati wa shambulizi hilo.
Awali  tuliweza kuzungumuza na mwakilishi wa kaunti katika wadi ya Arabia na kaweza kutuhakikishisa shambulizi hilo na vile vile alisema kuwa wanashuku wanamgambo wa Alshabab ndio waliofanya kitendo hicho.
Hadi sasa hakuna taarifa rasmi kutoka serikali kuhusiana na utekaji nyara na muda mfupi uliopita kulikuwa na taarifa isiyo thibitishwa kuwa chifu huyo ameuwawa na Alshabaab.
Kutokana na swala hili la Usalama wanasiasa jimbo la Mandera waliweza kuongea na wanahabari huku wakilaani kitendo hicho huku wakihimiza serikali kuimarisha usalama katika mkoa wa kaskazini mashariki mwa Kenya.

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments