.

.

Sinai ,Misri yashambuliwa

ZePLAN | 00:55:00 | 0 comments

Watu wapatao kumi na watatu wameuawa katika
katika mashambulio mawili yaliyotokea kwa
pamoja katika rasi ya Sinai nchini Misri.
Watu saba waliuawa na arobaini na wanne
kujeruhiwa wakati bomu lililokuwa limetegwa
katika gari kufyatuka katika kituo cha polisi
katika mji wa al-Arish.
Mapema, saa chache bomu lililokuwa limetegwa
pembeni mwa barabara liliwaua askari sita katika
mji wa Sheikh Zuweid.
Kundi linalojiita "Province of Sinai" yaani Jimbo la
Sinai --ambalo linachukuliwa kama tawi la
Islamic State -- limesema ndilo lililofanya
mashambulio yote mawili.
Wapiganaji wa kundi hili wamesema wanalipiza
kisasi dhidi ya serikali ya Misri ambayo
inawasaka wafuasi wa rais wa zamani wa Misri
aliyeondolewa madarakani, Muhammad Morsi.

Picha chini , jengo lililoshambuliwa na mabomu Sinai nchini Misri.

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments