.

.

Tanzania kushiriki mbio za kigali

ZePLAN | 01:18:00 | 0 comments

Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazotegemewa
kushiriki mbio za Kigali Marathon
zitakazofanyika May 23-24, huku nchi kadhaa
zikialikwa.
Michuano hiyo itakuwa ni ya wazi ya kimataifa,
kama yalivyo ya Kilimanjaro Marathon
yanayofanyika kila mwaka nchini Tanzania huku
wakimbiaji kutoka nchi mbalimbali kama vile
Kenya wakishiriki.
Kwa mujibu wa waandaaji, chama cha riadha
nchini Rwanda (RAF), mbio hizo za Kigali pia
zitakuwa na msisitizo wa kudumisha amani
kupitia michezo.wakimbiaji watashindana katika
mbio ndefu (kilometa 42) na half marathon
(kilometa 21) kwa upande wa wanawake na
wanaume. Mbio hizo zitaanza uwanja wa
Amahoro.
Wanariadha wengi kwa sasa wapo katika
matayarisho na mashindano mbalimbali
yakiwemo ya Olimpiki yatakayofanyika Rio de
Janeiro, Brazil mwaka 2016.

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments