Viongozi wa mataifa ya EU     
               
Jumuia ya muungano wa Ulaya imeiziomba mataifa sita, ambayo zamani yalikuwa ndani ya muungano wa usovieti,kuimarisha ushirikiano wao na mataifa ya Magharibi.
Rais wa baraza kuu la muungano wa Ulaya, Donald Tusk, amesema kuwa EU, imejitolea kuyasaidia mataifa hayo.
Viongozi wa ukraine na Latvia katika mazungumzo
Mataifa lengwa ni Armenia, Azerbaijan, Belarus, Georgia, Moldova na Ukraine.
Eu inasema kuwa inataka kuyasaidia dhidi ya ''mbinu potovu za unyanyanyasaji unaotumika na Urusi''.
Kando na mkutano huo, Waziri mkuu wa Ugiriki, Alexis Tsipras anafanya mkutano wa faragha ili kujadili namna ya kunusuru taifa lake lilnalosakamwa na madeni.
Rais wa baraza kuu la muungano wa Ulaya, Donald Tusk
Tsipras anajadiliana na viongozi wa Ufaransa Francois Ollande na Chansela wa Ujerumani Angela Merkel.
wakati huohuo Waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron, amesema kwamba ataanzisha mazungumzo kuhusiana na mpango wake wa kufanya mabadiliko katika jumuia ya bara Ulaya EU, atakapokutana leo na viongozi wa EU.
Cameron, ameahidi kuanzia mazungumzo ya mabadiliko katika EU
Anatabiri kutakuwa na pandashuka nyingi katika mazungumzo hayo, huku akisizitiza kuwa raia wa Uingereza watapiga kura ya maoni ya iwapo watajiondoa kutoka EU kabla ya mwaka 2017 au la.
Bwana Cameron amesema hayo baada ya kuwasili katika mji mkuu wa Latvia- Riga.
Viongozi wa mataifa ya jumuia ya bara Ulaya wamo kwenye mkutano unaolenga kuyaleta karibu na EU, mataifa sita ya uliokuwa muungano wa Usovieti