RUSIA:WHATSAPP YAPIGWA MARUFUKU
Kiongozi wa Chechnya Ramzan Kadyrov amewataka wanaume kuwazuia wake wao kutumia mtandao wa kijamii wa WhatsApp.
Kauli hiyo imefwatia mjadala mkali wa umma baada ya mada ya ndoa ya lazima kusambaa katika mtandao huo wa kijamii.Kadyrov amekaririwa akisema "wafungieni ndani, msiwaache wakatoka nje, hivyo hawatatuma chochote"
Kadyrov mapema aliunga mkono ndoa ya lazima kati ya afisa mkuu wa polisi na msichana wa miaka 17.
Afisa alikuwa anakiuka sheria ya Urusi.
Msaidizi wake mkuu amependekeza kuhalalisha ndoa za zaidi ya mke mmoja Chechnya.
Kiongozi huyo wa kiimla ni mshirika wa karibu sana wa Rais wa Urusi, Vladimir Putin, na katika miaka ya karibuni amepiga marufuku ndoa za lazima na ndoa zinazohusisha wasichana wenye umri mdogo.
Anamdhaniwa kuwa anaunga mkono ndoa za zaidi ya mke mmoja.
Pia anafikiriwa kuwa anapendelea ndoa za wake wengi.
Msaidizi wake mkuu Magomed Daudov anasema: "hiyo yote inaafikiana nasheria za dini ya Kiislamu ''Sharia''.
''Lakini kama mwanaume anaweza kumudu mahitaji ya mke zaidi ya mmoja, kwa nini asioe ?"
Asili mia kubwa ya raia wa jamhuri ya Chechnya ni Waislamu.
Kabla ya harusi hiyo ya jumamosi vyombo vya habari vilikuwa vimeripoti kuwa afisa huyo wa polisi Nazhud Guchigov, mwenye umri wa miaka 47, alikuwa amekanya Kheda Goylabiyeva asiondoke kwao
na hata akawatishia jamaa zake kuwa atawachukulia hatua kali endapo watamruhusu kuondoka.
Kheda Goylabiyeva alisimamiwa na msaidizi wa Kadyrov bwana Magomed Daudov alipokamilisha ndoa hiyo katika afisi za msajili.
Bwana Kadyrov, alisema kuwa wazazi wake msichana huyo walikuwa tayari wameshamruhusu kuolewa na afisa huyo mkuu wa polisi.
Kheda Goylabiyeva alifunga ndoa na Nazhud Guchigov katika mji mkuu wa Chechnya Grozny siku ya jumamosi.
Category:
0 comments