Liberia yafanikiwa kupambana na Ebola
Shirika la Afya Duniani, WHO, limetangaza rasmi kwamba hakuna tena Ebola nchini Liberia.
Taarifa ya WHO inasema, kuwa nchi hiyo haikupata mgonjwa wa Ebola kwa siku 42.
Rais wa Liberia, Ellen Johnson Sirleaf, alisema Liberia imefanikiwa, na itasherehekea juhudi za pamoja za kupigana na ugonjwa huo.
Liberia iliripoti kisa cha kwanza cha Ebola zaidi ya mwaka mmoja uliopita, wakati Ebola ilipoingia nchini humo kutoka nchi jirani ya Guinea.
Ugonjwa huo umewauwa watu zaidi ya elfu kumi na moja katika nchi za Afrika Magharibi; na ungaliko Guinea na Sierra Leone.
WHO imelaumiwa kuwa awali haikutia maanani onyo, kuhusu hatari za ugonjwa huo kuripuka, na kwamba shirika lilichelewa kuanza kuchukua hatua za kupambana nao.
Picha chini wauguzi wakuwa na nyuso za furaha baada ya mapambano juu ya ugonjwa huo kwa mda mrefu
Category:
0 comments