Rais wazamani wa Uturuki ameaga dunia
Aliyekuwa rais wa Uturuki Kenan Evren ambaye aliongoza mapindunzi yaliyokumbwa na umwagikaji wa damu mwaka 1980 ameaga dunia kwenye hospitali moja mjini Ankara akiwa na umri wa miaka 97.
Mwaka uliopita alihukumiwa kifungo cha maisha gerezani kufuatia kuhusika kwake kwenye mapinduzi ya kijeshi.
Chini ya utawala wake watu kadha walinyongwa , maelfu wakakamatwa na vyama vya kisiasa vikapigwa marufuku.
Vyombo vya habari vilivyotangaza kinyume na mapinduzi hayo vilifungwa . Generali Evren alidai kuwa alileta udhabiti nchini Uturuki.
Category:
0 comments