MISRI:Maandamano yazuka juu ya unyanyasaji wa kijisia nchini Misri
Shirika la kupigania haki za binaadamu lenye makao yake mjini Paris linasema kuwa vikosi vya usalama nchini Misri vinatumia unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wale wanaokomatwa na kuzuiliwa.
Shirika la International Federation for Human Rights linasema kuwa kumekuwa na ongezeko la visa vya dhuluma za kimapenzi tangu mapinduzi ya kijeshi yafanyike mwaka 2013.Linaushtumu utawala wa Misri kwa kutumia mbinu hiyo ili kuunyamazisha upinzani.
Wizara ya masuala ya ndani nchini Misri inasema kuwa haitazungumzia ripoti hiyo hadi ielewe kilicho ndani yake.
Category:
0 comments