SOUTH AFRICA: Rais Zuma aomba uchaguzi uhairishwe Burundi
Rais wa Afrika ya kusini Jacob Zuma amekuwa kiongozi wa hivi karibuni anayetaka uchaguzi wa urais nchini Burundi kuahirishwa.
Akizungumza baada ya mkutano wa kieneo nchini Angola,Bwana Zuma alisema kuwa uchaguzi huo haupaswi kufanyika hadi hali ya amani itakaporudi nchini humo.Maandamano yanaendelea katika mji wa Bujumbura kufuatia jaribio la mapinduzi la wiki iliopita.
Rais wa taifa hilo amekana madai ya kutaka kulipiza kisasi dhidi ya watekelezaji wa shambulio hilo.
Wafanyikazi wa mahospitali nchini Burundi awali walielezea kuwa kumekuwa na mshambulizi ya kulipiza kisasi ambapo polisi wamekuwa wakiwajeruhi wanajeshi waliodaiwa kuhusika na jaribio hilo.
Category:
0 comments