ABIRIA TAKRIBANI 300 WANUSURIKA KIFO
Hali imekuwa isio ya kufahamika baada ya tukio la janga la moto kuikumba meli iliokuwa ikifanya safari yake kutoka Unguja kuelekea Pemba ilio beba abiria takribani 300 nakuwaka moto
kutoka Zanzibar Meli aina ya Royal imeripotiwa kuungua moto na kuhatarisha maisha ya abiria ,ripoti inasema kuwa chanzo cha moto huo kimeanzia kwenye injini.
Lakini mpaka sasa hakuna taarifa kuhusu mtu hata mmoja ambae amefariki vifo .
Picha juu sehemu ya meli ilio athirika na moto |
Abiria walio valia maboya yakuogelea wakipatiwa msaada |
Hata hivyo abiria walipata msaada kutoka kwenye meli nyingine ya Serengeti iliyokuwa inatokea Pemba kwenda Unguja na kuweza kutoa msaada wa kwa abiria hao.
Category:
0 comments