KAULI YA RAIS WA TANZANIA DK JOHN POMBE MAGUFULI KUHUSU ELIMU BURE
Picha juu Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli |
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli amewahakikishia Watanzania kwamba elimu ya bure itapatikana kama alivyoahidi.
Amesema kuanzia mwezi huu fedha za kusomesha wanafunzi bure zitaanza kutengwa kuanzia mwezi huu.
Kwa mujibu wa Dkt Magufuli, Serikali imefikia uamuzi wa kutenga dola milioni 65.5, ambazo zitapelekwa moja kwa moja katika shule zenye uhitaji na kwamba fedha zitakapotumwa, nakala ya barua itapelekwa kwa mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya pamoja na mkurugenzi wake.
Rais Magufuli ameonya yeyote atakayetumia fedha hizo vinginevyo kwamba atachukuliwa hatua kali.
Mabadiliko yanawezekana Tanzania
Amesema fedha hizo zitasaidia katika ununuzi wa vitu kama vile chaki, maandalizi ya mitihani na vitu vingine vya muhimu shuleni.
Category:
0 comments