PEP GUARDIOLA ATAKA KUWEKA WAZI JUU YA MUSTAKABALI WAKE KUHUSU LIGI YA BUNDESLIGA
Picha juu kocha wa Bayern Munich Pep Guardiola |
Mkufunzi mkuu wa Bayern Munich Pep
Guardiola anasema kuwa ataelezea "wazi" kuhusiana na mustakabali wake
ligi ya Bundesliga juma lijalo.
Gazeti moja la Uhispania la Marca, limeripoti jana Jumatano kuwa Guardiola tayari ameiambia Bayern kuwa ataondoka klabu hiyo.
Gazeti hilo la Madrid linadai kuwa liaamini kuwa pande zote mbili, yeye pamoja na klabu, zitafaidika na mabadiliko hayo, kwa sababu bidii anayohitaji kutoka kwa wachezaji pamoja na mazoezi makali anayowafanyisha huenda yakaishia kuwaathiri.
Mwezi uliopita duru kutoka Uhispania zilidai kuwa mkufunzi huyo wa zamani wa Barcelona amekubali kuondoka Bayern mwisho wa msimu huu ili kuanza kuikufunza Manchester City.
Mabingwa hao wa Bavaria wamo kileleni kwa sasa ligi ya Ujerumani, alama tano mbele, wanapojiandaa kwa mechi yao ya mwisho ya mwaka 2015 ugenini Hannover Jumamosi.
Category:
0 comments