.

.

RAIA WA RWANDA WAPIGA KURA YA MAREKEBISHO YA KATIBA

ZePLAN | 11:01:00 | 0 comments

 Kagame

Rais wa Rwanda Paul Kagame ametetea uamuzi wa taifa hilo kuandaa kura ya maoni kuhusu muhula wa rais akisema lilikuwa wazo la Wanyarwanda.

Raia nchini humo wamepiga kura leo kuhusu marekebisho ya katiba ambayo huenda yakamuwezesha Bw Kagame kutawala hadi 2034.

Alipoulizwa na mwandishi wa BBC Catherine Byaruhanga kuhusu wazo la kubadilisha katiba, Bw Kagame alijibu: “Sikuomba hili lifanywe, nenda kawaulize Wanyarwanda mbona wakajiingiza katika hili.”

Bw Kagame hata hivyo alisema ukiangalia rekodi yake uongozini “labda unaweza kupata wazo na kujua ni yapi yanatarajiwa.”


Kiongozi huyo bado hajatangaza iwapo atawania tena baada ya muhula wake kumalizika 2017, na amesisitiza kwamba atatangaza hilo baada ya kura ya maoni.

Lakini kuhusu mipango yake ya siku za usoni kuhusu Rwanda amesema: “Wana (Wanyarwanda) mustakabali gani? Si mimi ninayedhibiti mustakabali wao. Wanashikilia hatima yao mikononi.”

Bw Kagame alipiga kura katika kituo cha Rugunga mjini Kigali.
Wapiga kura walikuwa wakipigia marekebisho ya katiba ya 2015, na miongoni mwa mengine kupunguza muda wa rais kuhudumu kuwa mihula miwili ya miaka mitano badala ya saba.
  Kagame
Raia 6 milioni walitarajiwa kupiga kura
Hata hivyo kutakuwa na kipindi cha mpito cha miaka saba kuanzia 2017 na Bw Kagame anaruhusiwa kuwania.
Hii ina maana kwamba anaweza kuongoza kwa miaka saba kuanzia 2017 kisha aongoze mihula miwili ya miaka mitano mitano, hadi 2034.

Kipindi cha maseneta kuhudumu pia kitaongezwa kutoka muhula mmoja wa miaka minane hadi mihula miwili ya miaka mitano mitano.

Mahakama za Gacaca, zilizoendesha kesi dhidi ya watuhumiwa wa mauaji ya kimbari ya 1994 pia zitavunjwa.
Mahakama hizo zimemaliza kazi baada ya kusikiza kesi dhidi ya watu 2 milioni.

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments