KWAMARA YA KWANZA WANAWAKE SAUDIA WARUHUSIWA KUPIGA KURA
Picha juu wanawake wa Saudia katika pilika pilika za uchaguzi |
Wapiga kura nchini Saudi Arabia
wanashiriki kwenye uchaguzi wa manispaa ambao pia ndio wa kwanza kwa
wanawake kukubaliwa kupiga kura.
Jumla ya wanawake 978 wamejitosa kuwania nyadhifa, pamoja na wanaume 5,938.
Wagombea wanawake walilazimika kuhutubu wakiwa nyuma ya pazia kwenye mikutano ya kampeni au kuwakilishwa na mwanamume.
Takriban wanawake 130,000 wamejiandikisha kupiga kura, maafisa wanasema.
Idadi hiyo ni ya chini sana ukilinganisha na wanaume wapiga kura, ambao kwa sasa ni 1.35 milioni.
Salma al-Rashed alikuwa mwanamke wa kwanza kujiandikisha kupiga kura.
„Nilihisi vyema sana,” alisema. “Mabadiliko ni neon kubwa lakini uchaguzi ndio njia pekee ya kuhakikisha tunawakilishwa katika uongozi.”
Uchaguzi huwa nadra sana Saudi Arabia, taifa linaloongozwa na mfalme, na uchaguzi huu wa Jumamosi ndiyo mara ya tatu kwa Wasaudia kupiga kura.
Hakukuwa na uchaguzi wowote kwa miaka 40 kati ya 1965 na 2005.
Uamuzi wa kuwaruhusu wanawake kushiriki uchaguzini ulifanywa na marehemu Mfalme Abdullah na uongozi wake unakumbukwa sana kwa hilo.
Category:
0 comments