MSANII DIAMOND PLATINUM AFANYA MAKUBWA ZAIDI
Msanii nguli nchini Nasibu Abdallah anatambuika kwa jina la Diamond Platinum ameachia nyimbo yake mpya inayotambulika kwa jina la " UTANIPENDA"
Nyimbo hiyo inaonekana kupokelewa vizuri na mashabiki kwakuwa imekuwa gumzo katika jiji la Dar es Salaam na mitaa yake kwa kuwa na wasikilizaji wengu zaidi na kuwa na watazamaji wengi kwenye mtandao wa youtube
Mpaka sasa msanii huyo anaongoza kwa kutwa tuzo nyingi zaidi nchini Tanzania za ndani na nje ya nchi .
Akiwashukuru mashabiki wake kwa kuwa nao mara zote katika kazi zake na kuonyesha kumjali kwa kusikiliza nyimbo na kununua kazi zake kitu ambacho kinamfanya yota huyu kuweza kupata maendeleo zaidi katika kazi yake ya sanaa.
Video hii ilireckodiwa katika mazingira tofauti tifauti ikiwa ni Tanzania na South Africa chni ya kampuni ya God Father ambayo imekuwa maarufu sana kwa kutengeneza video zenye ubora na kiwango cha kimataifa.
Ndani ya video hii ya utanipenda wameshirikishwa watu wakaribu zaidi na nyota huyu wa mziki akiwemo mama mzazi wa nyota huyo, PrincessTiffa mtoto wake na mkewe Zari au boss lady lakini watu wengine ni pamoja na boss Babu Tale na Jacline Wolper ambae ni nyota wa tamthilia za Tanzania ukitaka kuiona video hii pitia ukura wa youtube http/youtu.be/q9ll2ltDLsUk au unaweza kupata audio kupia tovuti ya Mikito.com .
Category:
0 comments