MADAKTARI KUPANDIKIZA UUME
Upasuaji umepangwa kufanyika kwa mara ya kwanza kupandikiza uume nchini Marekani, kwa lengo la kuwasaidia mpiganaji wa zamani
Upasuaji huo wa saa 12- utahusisha ushonaji wa neva muhimu na mishipa
ya damu kwa ajili ya kutunza mkojo na kumuwezesha mgonjwa kufanya tendo
la ngono.
Upasuaji huu unafuatia mafanikio ya kwanza kabisa ya upandikizaji wa uume nchini Afrika kusini mwaka jana.
Jopo
la madaktari kutoka Hospitali ya chuo kikuu cha Hopkins (JHU)
wanapanga kumfanyia upasuaji huyo mwanajeshi wa zamani mwenye umri wa
miaka 60kama sehemu ya majaribio.
Upasuaji wenyewe
Hatua ya
kwanza ya upasuaji huo itaanza kwa kuondoa uume kutoka kwa kijana
aliefariki ambaye alijitolea kutoa uume wake kwa ruhusa ya familia yake.
Kwa
mujibu wa jopo la madakatari katika JHU matumaini ya mwanajeshi huyo wa
zamani ni kwamba hisia za uume wake zitarejea katika muda wa miezi 12.
Uwezekano wa mgonjwa kupata watoto, utategemea kiwango cha jeraha na mafanikio ya upasuaji huo.
Lakini
Wanasayansi wanasema kutokana na kwamba ni upasuaji mmoja wa
kupandikiza uume uliofanyika, madaktari watakua makini kuhakikisha kuna
matumaini ya kweli.
Category:
0 comments