.

.

MICHEZO:Kocha wa Man U anena maneno matamu kuhusu Ryan Giggs.

ZePLAN | 21:53:00 | 0 comments

Kocha wa Manchester United Louis Van Gaal anaamini kwamba kilabu hiyo itamuajiri Ryan Giggs kama mrithi wake.
Giggs mwenye umri wa miaka 41 alisimamia mechi nne msimu uliopita baada ya aliyekuwa mkufunzi wa timu hiyo David Moyes kupigwa kalamu,kabla ya yeye kupewa kazi ya kuwa msaidizi wa Van Gaal.
Van Gaal ambaye atafikisha miaka 63 anakamilisha msimu wake wa kwanza kama kocha wa Man United na kandarasi yake inamalizika mwaka 2017.
Alipoulizwa kuhusu Giggs,kocha huyo aliiambia runinga ya kilabu hiyo kwamba anatumai kwamba ndiye atakayemrithi.
Giggs alisema kwamba alifurahi sana alipopewa jukumu la kuisimamia kilabu hiyo baada ya Moyes kupigwa kalamu

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments