.

.

MADIWANI WALIOFANYA VURUGU MKOANI TANGA KUFIKISHWA MAHAKAMANI

ZePLAN | 05:30:00 | 0 comments












Madiwani kadhaa wameripotiwa kufanya uvunjifu wa amani mkoani Tanga na kusabisha uharibifu wa mali za umma mkoani Tanga .

Kamanda wa polisi mkoani Tanga Zubery Mwombeji amesema madiwani 10 wa chama cha CUF watafikishwa mahakamani kama watabainika kuhusika na vurugu hizo.

Madiwani hao walikamatwa na kupelekwa kituo cha polisi cha Chumbageni kabla ya kuachiwa kwa dhamaana baada ya masaa machache hapo juzi, makosa wanayo husishwa nayo ni kosa la kuvunja mlango na kuchoma pazia kwenye ofisi ya mkurugenzi wa halmashauri.

Vurugu zilianza kutokea mara tuu baada ya jina la mshindi kutangazwa na mkurugenzi wa halmashauri bwana Daudi mayeji .

Mshindi wa kinyanganyiro hicho alikuwa ni mgombea wa Ccm kwa jina la Mohamed Mustafa (Selebosi) ambae alishinda kwa idadi ya kura 19 akifuatiwa na mpinzani wake ambae alipata kura 18.

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments