MAJESHI YA IRAQ YASEMA KUWA YANAKARIBIA KUUKOMBOA MJI WA RAMADI ZIDI YA IS
Majeshi ya Iraq yamesema kuwa
yanakaribia kuukomboa mji wa Ramadi baada ya kuanzisha mashambulizi
makali dhidi ya wapiganaji hao wa IS waliokuwa wakishikilia mji huo
tangu mwezi mei mwaka huu.
Balozi wa Iraq nchini Marekani Lukman Faily amesema majeshi ya serikali na washirika wake walikuwa katika hatua za mwisho za kushinda vita hivyo vya kuukomboa mji huo.
Hata hivyo msemaji wa jeshi la Marekani Colonel Steve Warren amekaririwa akisema kuwa bado kuna kazi kubwa katika mapigano hayo dhidi ya kundi hilo la kigaidi.
Category:
0 comments