MANENO ALIYOSEMA MOURINHO BAADA YA KUTIMULIWA CHELSEA
Sitokwenda likozo |
Jose Mourinho hataenda likizoni baada yake kufutwa na Chelsea Alhamisi.
“Hataenda likizoni, hajachoka, hahitaji likizo,” taarifa kutoka kwa wakala anayemwakilisha Mourinho imesema.
“Ana matumaini sana na tayari anaganga yajayo.”
Mourinho alijiunga na Chelsea kwa mara ya pili Juni 2013 na msimu uliopita akawaongoza kushinda Ligi ya Premia na Kombe la Ligi.
Hata hivyo Chelsea wamehangaika sana msimu huu.
Picha juu kocha Mourinho katika furaha baada ya kushinda kikombe |
"Jose Mourinho ana furaha kwamba alirejea Chelsea kwa sababu aliweza kuwapa mashabiki taji jingine la Ligi ya Premia, ligi ambayo hawakuwa wameshinda kwa miaka mingi,” taarifa ya Mourinho imesema.
“Anajivunia sana kushinda vikombe vinane akiwa Chelsea na anawashukuru mashabiki kwa muunga mkono vipindi hivyo viwili alikuwa katika klabu hiyo.
"Wakati wa maisha yake ya ukufunzi, Jose wakati mwingine amekuwa akiamua kuondoka katika klabu, lakini ni Chelsea pekee ambako klabu iliamua anafaa kuondoka.”
Chelsea watacheza mechi yao ya kwanza bila Mourinho Jumamosi, nyumbani dhidi ya Sunderland.
Category:
0 comments