HUKUMU YA KATANGA NA LUBANGA IMEPATIKANA KUFUNGWA JELA DR CONGO
Picha juu |
Hii ni mara ya kwanza kwa ICC kuwatuma wafungwa nje wakatumikie vifungo vyao.
Afisi ya Rais wa mahakama ya ICC ilitangaza DR Congo kuwa taifa litakalotumiwa kutekeleza vifungo vya wawili hao Desemba 8.
Mahakama ya ICC itaendelea kufuatilia kufungwa kwao kuhakikisha wanawekwa katika “mazingira yafaayo kimataifa ya kuwazuilia wafungwa”.
Picha juu Lubanga akiwa ICC |
Lubanga alihukumiwa kifungo cha miaka 14 jela tarehe 10 Julai, 2012 baada ya kupatikana na makosa ya kuwaandikisha watoto kwenye jeshi na kuwatumia vitani.
Mahakama ya rufaa ilidumisha hukumu hiyo Desemba 2014. Lubanga amekuwa kizuizini The Hague tangu 16 Machi 2006 na ukizingatia muda aliokaa kizuizini kabla ya kuhukumiwa, basi huenda akaachiliwa huru kabla ya 2020.
Picha juu Katanga akiwa ICC |
Katanga alihukumiwa kifungo cha miaka 12 jela kwa maoksa ya kushiriki kosa la uhalifu dhidi ya binadamu na makosa manne ya uhalifu wa kivita ya kuua, kushambulia raia na kuharibu mali kijiji cha Bogoro, Ituri mashariki mwa Dr Congo.
Anatarajiwa kukamilisha kifungo chake tarehe 18 Januari 2016.
Category:
0 comments