MAREKANI:WATU WAWILI WEUSI WAMEPIGWA RISASI NCHINI HUMO
Afisa mmoja wa polisi amewapiga
risasi watu wawili weusi alipoitwa kuchunguza kisa cha ugomvi wa
kinyumbani katika mji wa West Side Chicago nchini Marekani.
Wote wawili walikuwa weusi, huku familia zao zikilaumu idara ya polisi kwa kutumia nguvu kupita kiasi.
Msemaji wa polisi amesema kuwa kisa hicho cha kupigwa risasi kilifanyika baada ya maofisa walipokabiliwa na kile alichokitaja kuwa kushambuliwa.
Mamake mtu huyo anasema kuwa mwanawe hakuwa na bunduki alipopigwa risasi.
Naye mwanaye bi Jones anadai mamake alipigwa risasi punde tu alipofungua mlango uliokuwa unabishwa kwa nguvu na afisa huyo.
Polisi mjini Chicago wamelaumiwa kwa visa vya ubaguzi na mauaji yanayoegemea misingi ya ubaguzi wa rangi.
Mapema juma lililopita wenyeji wa mji huo waliandamana kupinga mauaji ya kijana mwengine mweusi aliyepigwa risasi 16 na afisa wa polisi mzungu.
Kisa hicho kiliibua hasira miongoni mwa wenyeji.
Category:
0 comments