MAFURIKO MAKUBWA NCHINI MAREKANI
Kimbunga kimepiga
jimbo la Texas nchini Marekani na kuezua mapaa ya nyumba, kuharibu
magari na kufanya baadhi ya maeneo ya mji wa Dallas kubakia katika giza
totoro.
Hali mbaya ya hewa imeathiri eneo kubwa la Marekani kusini katika msimu huu wa Krismasi, na kusababisha vifo vya watu 26.
Mataifa yaliyoathirika ni pamoja na Paraguay, Argentina, Brazil na Uruguay.
Mvua iliyonyesha mfululizo kwa siku kadhaa, imesababisha mito kufurika kupita kiasi, hasa katika maeneo tambarare ya nyanda za chini.
Wengi wa watu waliolazimika kimbilia usalama wao wanatoka katika maeneo ya mpakani katika mji wa Concordia, mahali ambapo viwango vya maji ya mto Uruguay, vimeongezeka maradufu.
Nchini Paraguay, taifa ambalo limeathirika zaidi, wakuu wanasema kuwa viwango vya maji vinaendelea kufurika.
Upepo mkali umeharibu nyaya za umeme, na kusababisha ukosefu mkubwa wa nguvu za umeme katika mji mkuu Asuncion, na maeneo mengine ya jirani.
Rais Mauricio Macri, atazuru eneo hilo hatimaye leo Jumapili.
Category:
0 comments