MASHITAKA YAWAKABILI VIOGOZI WA MAPINDUZI BURUNDI
Waziri wa zamani wa ulinzi nchini
Burundi Cyrille Ndayirukiye amefikishwa kortini akishtakiwa kupanga
mapinduzi dhidi ya serikali ya Rais Pierre Nkurunziza.
Wanadaiwa kupanga jaribio lililofeli la kupindua serikali ya Rais Pierre Nkurunziza mwezi Mei, upinzani dhidi ya hatua ya Bw Nkurunziza ya kuwania kwa muhula wa tatu ulipokuwa ukiongezeka.
Bw Ndayirukiye na washtakiwa wenzake wamemwambia jaji kwamba wamekuwa wakifungiwa katika “hali ya kinyama”, na wanalazimika kwenda haja kwenye ndoo.
Washtakiwa hao 28 wanadaiwa pia kuchochea mauaji na uharibifu wa mali.
Category:
0 comments