TUME YA KUPAMBANA NA UFISADI KENYA YA ONDOA TISHIO LA KUMKAMATA RAILA ODINGA
Picha juu kiongozi wa upinzani Raila Odinga |
Tume ya kupambana na ufisadi Kenya
imeondoa tishio la kumkamata kiongozi wa upinzani Raila Odinga kwa
sababu ya maelezo kuhusu jumla ya $1.3bn ($860m) ambazo anasema
zimetoweka serikalini.
Pesa hizo ni sehemu ya pesa kutoka kwa hati fungani za thamani ya $2.7bn ambazo ziliuzwa katika soko la hisa la Ireland mwaka jana.
Pesa hizo zilikusudiwa kutumiwa kwenye miradi ya miundo mbinu na pia kupunguza viwango vya riba kwa kutokopa sana pesa kutoka wakopeshaji nchini Kenya.
Bw Odinga alikuwa ametakiwa ajiwasilishe kwa tume hiyo kutoa maelezo zaidi la sivyo akamatwe.
Kiongozi huyo alikuwa amepinga hilo akisema hana habari zozote za kutoa kwa tume hiyo na badala yake wanafaa kupata melezo hayo kutoka kwa waliohusika katika kutoweka kwa pesa hizo.
Bw Odinga amemwambia mwandishi wa BBC Angela Ng'endo kwamba pesa za kukopwa kutoka nje zinafaa kutumiwa kwa miradi ya miundo mbinu pekee.
"Kuna mwanya wa Sh140bn ambazo inaonekana hazikufanya kazi yoyote. Ndizo tunauliza zilienda wapi. Kama ziliingia kwenye uchumi, ungehisi uzito wake," amesema.
Serikali imesisitiza kwamba matumizi yote yako wazi na hakuna pesa zilizotoweka.
Category:
0 comments