MSANII DAIMOND PLATINUM ATIKISA HADI NIGERIA WANANCHI WA NIGERIA KUMSUBIRI KWA HAMU KUBWA
Picha juu mwanamziki Nasibu Abdala (Diamond Platinum) |
Msani Diamond Platinum anaendelea kufanya vizuri zaidi katika mziki na hii inajidhihirisha sasa
kwamaendeleo yakupata show zaidi nchini Nigeria na mikoa yake.
Hali hii nichangamoto zaidi kwa wasanii wadogo wanao chipukia na wale walioanza mziki wao kwakipindi kirefu bila mafanikio niwapi warekebishe ili waweze kutangaza mziki katika nyanja za kimataifa.
Hali ya sasa inaonyesha mziki wa Tanzania umekuwa na wapenzi wengi zaidi kwa nchi za Afrika mashariki pamoja na Afrika magharibi na hii ni dalili nzuri kwakuwa wanatangaza zaidi Taifa la Tanzania pamoja na kufanya lugha ya kiswahili kutambulika nakuenea zaidi.
Picha juu waziri wa michezo, utamaduni na sanaa |
Wakati haya yote yanatokea waziri wa sanaa ,utamaduni na michezo Mh Nape Nauye ameanza kazi kwa kasi zaidi na kuahidi kulifanyia kazi swala zima la kazi za wasanii tatizo la wizi wa kazi za wasanii imekuwa kilio kikubwa sana na kasi hii inaleta matumaini na hari zaidi kwa wasanii wa mziki na filamu kuwapa hamasa katika kufanya kazi zao kwa ubora wa hali ya juu.
Category:
0 comments