MTOTO WA MFALME WA SAUDIA ATOA MAZITO JUU YA TRUMP
Picha ya mtoto wa mfalme wa Saudia |
Mwanamfalme
Alwaleed bin Talal wa Saudi Arabia amemshutumu mgombea urais wa chama
cha Republican Marekani Donald Trump kwa tamko lake kwamba Waislamu
wazuiwe kuingia Marekani.
Mwanamfalme huyo, ambaye ndiye mtu
tajiri zaidi katika ulimwengu wa Kiarabu, amesema Bw trumo anafaa kuacha
azma yake ya kutaka kuwa rais kwa sababu hawezi kushinda."Unaletea aibu chama cha Republican na Marekani kwa jumla," ameandika Bin Talal kwenye Twitter.
Bw Trump, mfanyabiashara tajiri kutoka New York, alikuwa amependekeza Waislamu wazuiwe kuingia Marekani kwa sababu za kiusalama.
- Mambo 20 makuu anayoamini Donald Trump
- Trump akemewa kwa matamshi kuhusu Waislamu
- US: Maneno ya Trump ni hatari kwa usalama
Amejibu matamshi hayo ya Bw Talal kwa kumuita mwanamfalme ”mjinga” na kumtuhumu kwa kutaka kufanya anachosema ni kutumia “pesa za baba” kudhibiti wanasiasa wa Marekani.
"Hutaweza kufanya hivyo nikichaguliwa," amemjibu Trump kupitia Twitter.
Category:
0 comments