SOMALIA: IDADI YA WATU ISIO JULIKANA WAMEKUFA KUTOKANA NA MLIPUKO WA BOMU
Picha juu mji wa Mogadishu kabla ya vita miongo miwili iliopita |
Watu kadha wameuawa kwenye shambulio la bomu na risasi katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu.
Picha juu kikosi cha Al-Shabab |
Shirika la habari la Reuters linasema watu watatu wamefariki.
Shambulio lilianza kwa ufyatuaji wa risasi na kisha bomu likalipuka polisi walipowasili, afisa wa polisi ameambia shirika la habari la AFP.
Haijabainika ni nani aliyehusika kwenye shambulio hilo.
"Wengi wa waathiriwa ni raia,” afisa wa polisi Ahmed Abdiweli ameambia AFP.
Picha juu hali ilivyo sasa |
Kundi la wapiganaji wa Kiislamu la Al-Shabab limetekeleza mashambulio kadha wiki za karibuni.
Category:
0 comments