UINGEREZA KUIONGEZEA NGUVU ZA KIJESHI AFGHANISTAN KUKABILIANA NA TALIBAN
Naibu gavana katika jimbo la Helmand
Kusini mwa Afghanistan amesema kuwa vikosi zaidi vya wanajeshi
vimewasili katika mji wa Sangin kusaidia mamia ya polisi na wanajeshi
waliozingirwa na wanamgambo wa Taliban.
Gavana wa Helmand alithibitisha mashambulizi hayo.
Mwandishi wa BBC aliyeko Kabul anasema kuwa vikosi vya usalama vimekuwa vikikabiliana na wapiganaji hao nje ya mji huo ila wameshindwa kuendelea mbele kutokana na mabomu ya kutegwa ardhini.
Taliban imechapisha ripoti kwenye mtandao wake ikisema kuwa inakaribia kutwaa kikamilifu mji wote wa Sangin.
Aidha wameilaumu majeshi ya Uingereza kwa kurejea mjini humo.
Walioshuhudia wamekuwa wakisema kuwa Taliban wamekuwa wakiwaua maafisa wa usalama baada ya kuyateka majengo ya serikali.
Mji wa Sangin awali ulikuwa kituo kikuu cha shughuli za NATO nchini Aghanistan.
Category:
0 comments