WANAWAKE WAISLAM WAWAFUNIKA WAKRISTO HIJABU KUWANUSURU NA AL SHABAAB
Mwalimu mmoja
aliyenusurika kifo katika shambulizi la basi lililotekelezwa na
wapiganaji wa Al shabaab hapo jana amesema kuwa wanawake wa
Kiislamu walivua hijab na kuwastiri wanawake wakristu ilikuwaokoa
wasiuawe.
''Walituambia kuwa sisi waislamu tulikuwa salama na hivyo tukang'amua kuwa wanawalenga wakristu''
''Hapo ndipo wanawake wakavua hijab zao na kuwastiri wanawake wakristo''.
''Kwa sababu walikuwa ni wanaume ,wanawake walijitenga na kuwaficha wanawake wakristo na hivyo kuwaokoa wasiuawe'' alisema mwalimu huyo ambaye anauguza majeraha mjini Mandera.
''Ilikuwa vigumu kutambua nani ni muislamu na nani siye''
Category:
0 comments