RAIS JOHN POMBE MAGUFULI AKUTANA USO KWA USO NA MAALIM SEIF SHARIF HAMAD IKULU
Picha juu Rais wa Tanzania J.P Magufuli alipo kutana na Seif |
Kiongozi wa chama
kikuu cha upinzani nchini Zanzibar-CUF Maalim Seif Hamad amefanya
mazungumzo na rais John Magufuli wa Tanzania katika harakati za kujaribu
kusuluhisha mzozo wa kisiasa unaokumba kisiwa hicho.
Katika taarifa kutoka ikulu ya Dar es Salaam rais Magufuli alimshukuru Dr Ali Shein na Maalim Seif kwa jukumu la kutafuta amani kisiwani humo.
Hata hivyo, baadhi ya viongozi wa upinzani wamekashifu mkutano huo na kusema kwamba mazungumzo yoyote kuhusu mzozo wa Zanzibar yafaa yawahuhishe viongozi wote.
Mwenyekiti wa chama cha upinzani cha kijamii CCK Constantine Akitanda aliisema kuwa upinzani ulipaswa kujumuishwa kwa pamoja kama washirika wa uchaguzi mkuu uliotibuka wa kisiwa cha Zanzibar.
Akitanda alisema kuwa viongozi wakuu wa vyama vyote na tume kwa pamoja na rais wanapaswa kujadili mstakabal wa kisiwa hicho kisiasa.
'je watajadili wawili pekee yao ilhali wanapanga uchaguzi utakaotuhusisha sisi sote ?''
Haipaswi kuwa hivyo alisema Akitanda.
- Kisiwa cha hicho kilitumbukia katika mzozo wa kisiasa baada ya tume ya uchaguzi kufutilia mbali matokeo ya uchaguzi huo ikisema kuwa haukuwa wa haki na kwamba kulikuwa na ukiukaji mkubwa wa sheria za uchaguzi.
Kadhalika, kura zilidaiwa kuwa hazikupata ulinzi mzuri hususan kisiwani Pemba ambako baadhi ya mawakala wa vyama vya siasa katika kisiwa hicho walifukuzwa.
Vilevile vijana walidaiwa walivamia vituo vya kupigia kura kwa lengo la kutaka kuzua ghasia, na pia vyama vya siasa vilionekana "kuingilia majukumu ya tume ikiwemo kujitangazia ushindi na kupelekea mashindikizo kwa tume."
Category:
0 comments