WAWILI WAKAMATWA PARIS
- Yamkini waliokamatwa ni afisa mmoja mstaafu wa polisi ambaye ni mshukiwa mkuu huku mkewe akitumika kama shahidi.
- Mkurugenzi mkuu wa shirika la ndege la Air France alifutilia mbali tahadhari ya' bomu' iliyosababisha ndege ya kutua Kenya kuwa ni bandia.
Ndege hiyo ya Ufaransa chapa Boeing 777 nambari AF463 inayohudumu kati ya Mauritius na Paris ililazimika kutua baada ya kile kinachotajwa kuwa bomu bandia.
Inasemekana kuwa abiria mmoja alikipata kifaa hicho chooni na akamfahamisha mhudumu mmoja wa ndege hiyo.
Ndege hiyo ilitua saa sita usiku wa kuamkia Jumapili, huku wataalamu wa kutegua mabomu kutoka jeshi la wanamaji la Kenya wakiingia ndani ya ndege hiyo kukagua kifurushi kilicholeta taharuki.
Sasa kitengo cha ujasusi cha Ufaransa kimeanzisha uchunguzi wa kina kubaini kilichosababisha tishio hilo.
Category:
0 comments