SYRIA: MASHAMBULIZI YA ANGA YAMERIPOTIWA KUTOKEA LEO
Maelfu ya watu wameuawa upande wa
kaskazini-magharibi mwa Syria katika mfululizo wa mashambulizi ya anga
yaliyotokea katika mji wa Idlib.wakaazi wa mji huo wamesema kwamba eneo
la soko, makaazi ya watu, na majengo kadhaa yamegongwa .
Nao wenyeji wa mji huo wameeleza kuwa mashambulizi hayo ya anga yamefanywa na ndege za kivita za majeshi ya Urusi,ingawa mpaka sasa Urusi yenyewe haijathibitisha juu ya suala hilo.
Kwingineko,runinga ya taifa la Syria imetoa taarifa kuwa watu kumi wamejeruhiwa wakiwa katika basi la jeshi katika mji mkuu wa nchi hiyo , Damascus.
Category:
0 comments