Rais wa Somalia Hassan Sheikh
Mohamoud amesema kuwa takriban wanajeshi 180 wa Kenya waliuawa katika
uvamizi wa kambi yao huko al-Ade na wapiganaji wa kundi la al-Shabab.
''Wanajeshi
wa kigeni hufariki na hatuendi katika mazishi yao. Wakati wanajeshi 180
ama 200 wa Kenya waliotumwa nchini Somalia na sababu ya kutumwa kwao
nchini humo ni kuleta uthabiti kuwasaidia raia wa Somalia na wanauawa
alfajiri moja, si jambo la kawaida kwamba wageni wameuawa," amenukuliwa
Rais Mohamoud na kituo kimoja cha runinga nchini Somalia.
"Kile kilichosalia ni kwamba jamaa zao walielezwa kwamba kulikuwa na vita na watu wao wakafariki kutokana na hilo."
Taarifa kutoka kwa maafisa wa jeshi la Kenya ambao bado hawajazungumzia habari hizi.
Mazishi ya wanajeshi waliouawa yamekuwa yakifanyika maeneo mbalimbali Kenya
Baada ya shambulio hilo kutokea tarehe 15 Januari, Rais Kenyatta aliahidi kwamba majeshi ya Kenya
yange waandama waliohusika.
Category:
About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!
Related posts:
If you enjoyed this article, subscribe to receive more just like it.
0 comments