NDEGE ILIOBEBA WATU 23 IMETOWEKA NEPAL
Maafisa wa uokoaji wamepata mabaki ya ndege hiyo |
Ndege ndogo iliyowabeba watu 23 imetoweka ikiwa maeneo yenye milima nchini magharibi mwa Nepal.
Ripoti zinasema mabaki ya ndege hiyo yamepatikana ingawa hakuna habari kuhusu majeruhi au manusura.Ndege hiyo ilikuwa safarini kutoka Pokhara, magharibi mwa mji mkuu Kathmandu, kwenda Jomsom, eneo ambalo watu wengi wanaoenda kukwea milima ya Himalaya huanza safari yao ya kukwea milima hiyo.
Ndege hiyo ilipoteza mawasiliano na maafisa wa udhibiti wa safari za ndege wa Pokhara dakika 10 baada ya kupaa.
Hakuna viwanja vya ndege kati ya maeneo hayo mawili na inahofiwa kwamba ndege hiyo imeanguka.
Ajali za ndege hutokea mara kwa mara nchini Nepal.
Tangu mwaka 1949, kumetokea zaidi ya ajali 70 zilizohusisha ndege za kawaida na helikopta, na vifo vya watu 700.
Category:
0 comments