INDONESIA:JUA LAPATWA NCHINI INDONESIA KWA MUDA MREFU ZAIDI HAIJAWAHI KUTOKEA
Indonesia ndio nchi pekee iliyoshuhudia tukio hilo kote duniani.
Mamia ya watu walimiminika kushuhudia jua likinaswa na mwezi
Katika kisiwa cha Belitung mamia ya wageni na watalii wa
nchini walikusanyika katika fukwe za bahari kabla ya alfajiri. Wakati jua
lilipoanza kunaswa na mwezi walishangilia na baadaye kunyamaza kimya
kwa mshangao.
Wengi wamelielezea tukio hilo kama 'tukio la
miujiza'. Kwa wengi Indonesia, tukio hilo linashirikishwa sana na dini
na watu huomba, sherehe za kitamaduni na ngoma zimeandaliwa katika
sehemu kubwa la eneo hilo.
Wanasayansi pia walikuwepo
katika eneo la Maba katika visiwa vya Maluku ambako tukio hilo
limeshuhudiwa kwa Dakika tatu, ambao ni muda mrefu kuwahi kushuhudiwa
jua likinaswa na mwezi.
Category:
0 comments