.

.

RAIA WA MAREKANI AUWAWA ISRAEL KWA KUCHOMWA KISU

ZePLAN | 04:20:00 | 0 comments

Raia wa Marekani ameuawa kwa kudungwa kisu katika eneo la Jaffa nchini Israeli. Shabulio hilo limetokea wakati makamu wa rais wa Marekani Joe Biden alipokuwa anakutana na aliyekuwa rais wa Israel Shimon Peres katika kituo cha amani cha Peres kilichopo karibu na eneo hilo.

Raia kadhaa wa Israel pia walidungwa visu na kujeruhiwa vibaya.
Taarifa ya Biden imesema ameshutumu vikali alichokitaja kuwa 'shambulio baya'.

Makamu wa rais Marekani Joe BIden ameshtumu shambulio hilo
Awali kulikuwa na mashambulio Jerusalem na Israel katikati.
Mshambuliaji alielekea Telaviv na kuchoma visu watu wengine kadhaa kabla ya kupigwa risasi na kuuawa.

Polisi wa Israel wamesema alikuwa raia wa Paletina kutoka ukingo wa magharibi.
Kumeshuhudiwa ongezeko la mashambulio
Saa chache baadaye raia watatu wa Israeli walijeruhiwa katika mashambulio mengine mawili tofauti Mashariki mwa Jerusalem na Petah Tikva . Katika matukio yote washambuliaji wameuawa.

Tangu Oktoba, Kumeshuhudiwa ongezeko la mashambulio Israel na maeneo ya Palestina yaliosababisha vifo vya zaidi ya raia 180 wa Palestina na takriban Waisraeli 30.

Maafisa wa serikali Israeli wanasema wengi wa raia hao wa Palestina waliuawa wakiwa katika kutekeleza mashambulio ya kutumia visu bunduki au kugonga watu kwa gari.

Wengine wameuawa katika makabiliano na vikosi vya usalama vya Israeli . Joe Biden anatarajiwa kukutana na viongozi wa Israeli na Palestina Jumatano.

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments