KANALI WAJESHI AFUNGWA JELA MIAKA 21
Aliyekuwa kamanda
mkuu wa kikosi cha ulinzi wa Rais Paul Kagame, Kanali Tom Byabagamba,
amehukumiwa kifungo cha miaka 21 jela na kuvuliwa cheo chake baada ya
kupatikana na hatia ya kuharibia sifa nchi hiyo na kuhamasisha wananchi
kupinga utawala.
Maafisa hao wa jeshi wamepinga hukumu hiyo wakisema mashtaka dhidi yao yalichochewa kisiasa.
Mahakama imeunga mkono hoja za upande wa mwendesha mashtaka kwamba mlinzi wa muda mrefu wa Rais Kagame, Kanali Byabagamba, alihusika na makosa matatu ambayo ni kueneza kampeni za chuki dhidi ya utawala ambazo zingesababisha wananchi kugoma dhidi ya serikali ya nchi hiyo na kutoheshimu bendera ya nchi hiyo.
Brigedia jenerali mstaafu Frank Rusagara naye amepatikana na makosa kama hayo pamoja na kosa la kumiliki silaha kinyume cha sheria.
Awali alikiri kumiliki bastola mbili alizopewa kama zawadi na nchi za Afrika Kusini na Israel, wakati alipokuwa afisa mkuu anayehusika na ununuzi wa silaha katika wizara ya ulinzi ya Rwanda.
Maafisa hao wamekata rufaa baada ya mahakama kutangaza hukumu hiyo.
Category:
0 comments