Hatua ya mchezaji
maarufu wa soka duniani Lionel Messi kutoa viatu vyake viuzwe kusaidia
watu wasiojiweza imeibua mjadala mkali nchini Misri.
Messi
alifanya hivyo akidhani labda kwamba alikuwa anafanya hisani bila
kufahamu kwamba viatu huwa na maana nyingine nchini Misri na pia katika
mataifa ya mengine ya Uarabuni.
Wakati wa mahojiano ya runingani
''katika kipindi cha Yes am Famous'' kinachopeperushwa hewani na runinga
ya MBC Misri, mchezaji huyo wa Argentina aliwaambia watangazaji hao
kwamba angependa kutoa viatu vyake vipigwe mnada.
Kitendo chake
kilipokelewa tofauti kabisa na wiki chache zilizopita alipopongezwa na
kusifiwa sana kwa kutimiza ndoto ya kijana mmoja wa Afghanistan
alipomtumia mpira na fulana yake.
Mchezaji Lionel Messi katikati
Alipokuwa akivitoa viatu vyake Misri, hakujua kwamba
viatu huchukuliwa kama matusi au kukosea watu heshima katika maeneo
mengi ya Mashariki ya Kati.
Muda mfupi baadaye wakazi wa maeneo hayo walimkashutumu sana kupitia mitandao ya kijamii.
Mbunge aliyetoa viatu vyake ili kumpatia MessiNa ili kujibu matusi hayo mbunge mmoja wa Misri said
Hassin anayetangaza kipindi kwa jina 'Infirad' alitoa kiatu chake na
kusema kwamba atampatia Messi.
Category:
About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!
Related posts:
If you enjoyed this article, subscribe to receive more just like it.
0 comments