TANZANIA:RIPOTI YA MADAWA YA KULEVYA YAZINDULIWA NA (UNIC). BANGI,MIRUNGI,HEROIN VYASHIKA NAMBA
Kituo
cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) kimezindua ripoti ya Bodi ya
Kimataifa ya Kuzuia Madawa ya Kulevya (INCB) na kuelezea hali ya
matumizi ya madawa ya kulevya ilivyo nchini na hatua zinazotakiwa
kuchukuliwa.
Akisoma
ripoti hiyo, Mkuu wa Elimu, Habari na Takwimu kutoka Tume ya Taifa ya
Kudhibiti Dawa za Kulevya, Amani Msami alisema katika ripoti hiyo
inaonyesha kuanzia mwaka 2014 biashara ya Bangi, Mirungi na madawa ya
kulevya aina ya Heroin yaliongezeka na katika kipindi cha mwaka 2013
zaidi ya Kilo 321 za Heroin zilikamatwa nchini.
Alisema
nchi za Afrika Mashariki zimekuwa zikitumika kama sehemu ya kupitishia
madawa kwenda maeneo mengine ya dunia ambapo dawa hizo zimekuwa
zikitokea nchi za Afghanstan, India, Iran na Pakistan na kupelekwa nchi
kama China, Japan, Afrika Kusini, Marekani na nchi zingine za Ulaya.
Aliongeza
kuwa madawa hayo yamekuwa yakipitishwa nchini kwa kutumia meli kubwa
ambazo zimekuwa zikitumia majahazi, mashua, ngalawa na boti ziendazo
kasi ili kufikisha madawa ya kulevya nchi kavu.
Aidha
alieleza kupitia ripoti hiyo inaonyesha kuwa katika kila watu 100
barani Afrika, watu 8 wanakuwa wanatumia bangi na hivyo kuifanya bangi
kuongoza kwa matumizi makubwa Afrika na zaidi matumizi ya bangi ipo nchi
za Afrika Magharibi na Afrika ya Kati.
Madawa
mengine yanayoongoza kwa matumizi makubwa Afrika ni pamoja na madawa
aina ya Heroin ambapo katika watu 1,000 watu 3 wanatumia madawa hiyo na
Cocaine inashika nafasi ya tatu kwa matumizi makubwa.
Pia
alisema kuwa ripoti imezitaja nchi za Tanzania, Kenya na Senegal kwa
kuanza kutoa huduma ya kuwapa waathirika wa matumizi ya dawa za kulevya,
dawa za Methadone ambazo zinasaidia kuwarudisha waathirika katika hali
zao za awali.
“Ripoti
hii inaonyesha jinsi hali ilivyo na Tanzania kama nchi wanachama
inatakiwa ifanye baadhi ya marekebisho ili kuzuia biashara na matumizi
na hawa wafanya biashara wa haya madawa wanatumia sana watu wenye kipato
cha chini na wakifikisha mizigo yao wanawalipa,” alisema Msami.
Nae
Afisa wa Umoja wa Mipango wa Umoja wa Mataifa anayesimamia udhibiti wa
dawa za kulevya na uhalifu unaosababishwa na madawa ya kulevya,
Immaculate Maliyamkono alisema ripoti imeyotolewa na INCB inaonyesha
kuwa bado kuna biashara ya madawa za kulevya kwa nchi za Afrika
Mashariki na hivyo ni wajibu wao kama wanachama wa bodi hiyo kuangalia
upya sera zao ili kudhibiti biashara na matumizi ya madawa ya kulevya.
“Kama
ripoti imevyoonyesha INCB inawataka wanachama wake wafanye sawa na
mkataba wa mwaka 2009 ili kuzuia biashara ya haya madawa na hatua
zinazoweza kuchukuliwa ni pamoja na kubadili sera inayotumika sasa,”
alisema Bi. Maliyamkono.
Afisa
Habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Stella Vuzo
akizungumza kuhusu ripoti ya INCB kuhusu madawa ya kulevya. Kulia
ni Afisa wa Umoja wa Mipango wa Umoja wa Mataifa anayesimamia udhibiti
wa dawa za kulevya na uhalifu unaosababishwa na madawa ya kulevya,
Immaculate Maliyamkono.
Mkuu
wa Elimu, Habari na Takwimu kutoka Tume ya Taifa ya Kudhibiti Dawa za
Kulevya, Amani Msami akisoma ripoti ya Bodi ya Kimataifa ya Kuzuia
Madawa ya Kulevya (INCB).
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo.
Afisa
wa Umoja wa Mipango wa Umoja wa Mataifa anayesimamia udhibiti wa dawa
za kulevya na uhalifu unaosababishwa na madawa ya kulevya, Immaculate
Maliyamkono. Mkuu wa Elimu, Habari na Takwimu kutoka Tume ya Taifa ya
Kudhibiti Dawa za Kulevya, Amani Msami (kulia) na Afisa Habari wa kituo
cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Stella Vuzo (kushoto).
Mkemia
Mkuu wa Tume ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Yovin Ivo akizungumza jambo
kuhusu madawa ya kulevya. Kushoto ni Mkuu wa Elimu, Habari na Takwimu
kutoka Tume ya Taifa ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Amani Msami.
Uzinduzi wa Ripoti ya Bodi ya Kimataifa ya Kuzuia Madawa ya Kulevya (INCB) ukifanyika.
Category:
0 comments