Home �
� KOREA KASKAZINI YAFANYA MAJARIBIO YA MTAMBO WAKE WA SILAHA TENA
ZePLAN |
16:07:00 |
0
comments
Korea Kaskazini imesema kuwa
imefanikiwa kufanya majaribio ya mtambo wake mpya, ambao unaweza kurusha
makombora kutoka bara moja hadi jiingine, katika juhudi za kuimarisha
uwezo wake wa kufanya mashambulio dhidi ya Marekani.
Vyombo vya habari vya Korea Kaskazini vinasema kuwa zoezi hilo liliongozwa na kiongozi wa taifa hilo Kim Jong-un.
Jaribio
hilo ni katika harakati za hivi karibuni za utawala wa Pyongyang wa
kuunda zana za nuklia tangu ilipofanya jaribio lake la nne la makombora
ya nuklia January mwaka huu.
Hatua hiyo iliiushurutisha Umoja wa Mataifa kuiwekea Korea Kaskazini vikwazo vipya.
Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imetoa wito kwa utawala wa Pyongyang kujiepusha na vitendo vyake vya uchochezi.
Category:
About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!
0 comments