Baada ya milipuko mitatu iliyotokea mapema leo Machi 22.2016 nchini Ubelgiji katika mji Mkuu wa nchi hiyo iliyotokea kwenye reli ya chini kwa chini, kituo cha treni cha Metro na uwanjwa wa ndege wa Brucesels huku watu zaidi ya 30 kulipotiwa kupoteza maisha na wengine kujeruhiwa, timu ya soka anayochezea Mtanzania Mbwana Samatta imetoa neno.

Kupitia ukurasa wa mtandao wa kijamii wa facebook wa klabu ya KRC Genk  uliweza kuandika maneno ya kuwatia moyo ndugu na jamaa waliopatwa na msukosuko huo  pamoja na wale waliopoteza maisha.

beg
Ramani ya inayoonyesha mji Mkuu wa Brussels na mji wa Genk


“Timu yetu ya Genk inaungana kutoa msaada kwa wale wote ambao wameathirika na mashambulizi ya kutisha katika mji Mkuu wa Brussels.  Genk kauli yetu ni kuwa Tunawatakia ngvu, Uhodari na umoja” ulieleza ujumbe huo na kumalizia neno la kuiombea Taifa hilo la  prayforbelgium

Umbali kutoka mji Mkuu wa  Brussels hadi katika Mji wa Genk kwa usafiri wa trni ni muda wa saa moja huku kwa ndege za kawaida ni dakika kadhaa licha ta klabu ya Genk kuwa na michezo muhimu hapo mbele itakayopigwa hapo baadae imeendelea kutoa rai kwa kuhimiza suala la amani duniani kote..

Hata hivyo, Mtanzania Mbwana Samatta tayari yupo nchini Chad, akiwa tayari kukiongoza kikosi cha timu ya Taifa cha Tanzania ‘Taifa Stars’ ambacho kinatarajiwa kushuka dimbani hiyo kesho Machi 23.2016.

CeJxkVAXIAEo0WB (1)
Picha iliyowekwa na klabu ya Genk iliyokuwa na kauli mbiu;prayforbelgium