PAKA MWIZI WA NGUO ZA NDANI HUYU HAPA
Paka mmoja mwizi wakati wa usiku amekuwa akiiba soksi pamoja na nguo za ndani nchini New Zealand.
Katika
kipindi cha miezi miwili, paka huyo mwenye umri wa miaka sita kwa jina
Brigit kutoka mji wa Hamilton aliiba suruali za ndani 11 na zaidi ya
soksi 50.
Mmiliki wake Sarah Nathan alichapisha tabia ya paka huyo isiyo ya kawaida katika mtandao wake wa facebook.
''Tabia
hiyo sasa inazidi kuwa mbaya.Lazima kuna mtu ambaye anakosa vitu
vyake'',alisema katika chapisho lake la ukursa wa facebook
lililosambazwa mara 500.
Bi Nathan amesema kwamba tatizo lilianza alipogundua vipande kadhaa vya nguo za ndani katika nguo zake anapoziosha.
''Suruali
hizo za ndani hazikuwa zetu,na siku moja Brigit aliingia katika chumba
cha wageni akiwa amebeba soksi aliongezea'',akisema kuwa waathiriwa wa
Brigit walikuwa majirani katika nyumba za ghorofa.
Category:
0 comments