UMOJA WA WANAWAKE WAZINDUA KUNDI LA HEFORSHE IKIWA NA LENGO LAKUWEKA USAWA WA KIJINSIA
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez
akitoa hotuba katika mdahalo kuhusu wanawake na uzinduzi wa Kundi la
`HeForShe`.
Umoja wa Mataifa Wanawake (UN Women)
nchini umefanya uzinduzi wa kundi la mshikamano la Kimataifa
linalohusisha wanaume na wavulana lililo na malengo ya kuhakikisha
kunapatikana usawa wa kijinsia baina ya wanaume na wanawake ‘HeForShe’.
Akizindua kundi hilo, Mratibu Mkazi wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo
(UNDP), Alvaro Rodriguez alisema usawa kijinsia ni haki ya kila binadamu
na kupitia kundi hilo ni wajibu wa kila mwanaume na mvulana kusaidia
kupatikana kwa usawa kwa wanaume na wanawake katika maeneo yote ambayo
yanaonekana kuwa na upendeleo kwa upande mmoja.
“Usawa wa kijinsia sio tu suala la
wanawake pekee, ni suala la haki za binadamu ambalo hutuathiri sisi
sote. Usawa wa kijinsia sio tu kuwawezesha wanawake, lakini pia huweka
huru watu kutoka katika ubaguzi uliowekwa kijamii na majukumu ya
kijinsia,” alisema Rodriguez.
Awali Balozi wa Sweden nchini, Katarina
Rangnitt alieleza kuwa usawa wa kijinsia unahusisha pia katika kusimamia
shughuli mbalimbali ikiwepo za nyumbani kwa wanaume na wanawake
kushirikiana kuzifanya kwa pamoja.
Alisema ni muhimu kwa jamii kuelewa kuwa
ni jambo lenye maana kuwepo kwa usawa wa kijinsia ili wanawake nao
waweze kusaidia shughuli za maendeleo kwa familia na taifa kwa ujumla.
“Usawa uwepo katika sehemu zote hata kazi
za nyumbani zifanyike kwa pamoja … ni muhimu kwa mama, baba na kijana
kuwepo kwa usawa wa kijinsia kwa watu wote,” alisema Bi. Rangnitt.
Siku ya Wanawake kwa mwaka huu kidunia
imekuwa na kauli mbiu ya kimataifa isemayo ‘Dunia 50-50 Ongeza Jitihada
kwa ajili ya Usawa wa Kijinsia’ na kitaifa kaulimbiu imekuwa ni ’50-50
ifikapo 2030 Tuongeze Jitihada’.
Balozi
wa Sweden nchini, Katarina Rangnitt (wa kwanza kulia), Mratibu Mkazi wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo
(UNDP), Alvaro Rodriguez na Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa wa Wanawake
nchini, Anna Collins-Falk
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akizindua Kundi la Mshikamano la
`HeForShe`.
Mdahalo ukiendelea, (wa kwanza kulia)
Katibu Mkuu wa Bazara Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC),
Beng`i Issa, Kiongozi wa Timu ya Umoja wa Mataifa wa Wanawake ya
Uwezeshaji Kiuchumi, Mehjabeen Alarakhia na Mshauri wa Jinsia na
Maendeleo, Edward Mhina.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akitoa hotuba katika mdahalo kuhusu
wanawake na uzinduzi wa Kundi la `HeForShe`.
Balozi wa Sweden nchini, Katarina Rangnitt.akitoa hotuba kuhusiana Siku ya Wanawake.
Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa wa Wanawake nchini, Anna Collins-Falk
Mshereheshaji wa mdahalo huo, Usu Mallya
Mwakilishi
wa Umoja wa Mataifa wa Wanawake nchini, Anna Collins-Falk akikata keki
ya kusherekea Siku ya Wanawake Duniani, Kushoto ni Mratibu Mkazi wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo
(UNDP), Alvaro Rodriguez.
Category:
0 comments