UTATA VIFO VYA WATU WATATU MBEYA
Hatimaye
kitendawili cha watu watatu walionyongwa kisha kuchomwa moto kwenye
Gesti ya Mexico mjini Kyela, kimetenguliwa baada ya ndugu kujitokeza na
kuwataja kwa majina halisi.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi alisema baada ya vyombo vya
habari kuandika tukio hilo, ndugu na jamaa wa marehemu walijitokeza na
kugundua majina waliyoandika na maeneo wanayotoka ni uongo.
Msangi
alisema ndugu wa marehemu baada ya kusoma na kusikia kwenye vyombo vya
habari, walianza kuwapigia simu jamaa zao na mmoja wao aligundua kwamba
ndugu yake anayeitwa Rogers Mwaka (49), ambaye ni Wakala wa Kampuni ya
Vodacom hapatikani na hakuonekana nyumbani.
“Kwa
mtandao huo pia tuliweza kufanikiwa kuwapata ndugu wa marehemu wengine,
ambao wamewatambua kwa alama na majina yao halisia,” alisema.
Alisema
mwanamke aliyeuawa kwenye tukio hilo na kutambuliwa kwa jina la Mariam
Hassan, kwa sasa ametajwa kwa majina halisi kwamba ni Zauda Hussein
Omary mzaliwa wa Mbarali na mkazi wa Veta jijini hapa wala hatoki
Songea.
Msangi
alisema marehemu mwingine ametambuliwa kwa jina la Baraka Chaula (27),
ambaye ni mdogo wa Zauda kutokana na kuchangia mama, lakini baba tofauti
na mkazi wa Mbarali alikuwa akifanya kazi za kilimo na biashara.
Akizungumza
kwa uchungu ndugu wa marehemu Zauda na Baraka, aliyejitambulisha kwa
jina la Riziki Chaula mkazi wa Mbarali, alisema alifika Kyela baada ya
kugundua simu za mdogo wake hazipatikani.
Riziki
alisema Zauda ni mke wa Abdallah Malifyuma, anayeishi Mbeya na kwamba
alimuaga mumewe kwamba alikuwa akielekea Tukuyu wilayani Rungwe
kibiashara.
Mkazi
wa Ilomba jijini hapa, Sebastian Amani ambaye alifika Kyela alisema
aliamua kupanda gari baada ya simu za Rogers kutopatikana licha ya kuaga
kwamba anakwenda Chunya.
Amani alisema chanzo cha mauaji hayo hakijajulikana na kwamba yamewaweka kwenye wakati mgumu jinsi yalivyotokea.
Jana
hiyo, Riziki alishirikana na mume wa Zauda, Malifyuma kuchukua miili ya
marehemu hao wawili ilhali Aman ‘akibeba msalaba’ wa kusafirisha mwili
wa Rogers.
Category:
0 comments