MAREKANI NA CHINA WAKOSA USINGIZI JUU YA KOREA KASKAZINI WAKAA VIKAO KUJADILI
Korea kaskazini imekuwa gumzo wakati wa mkutano wa dunia juu ya usalama wa nyuklia unaofanyika mjini Washngton.
Hali ya wasiwasi imetanda juu ya jaribio la Korea kaskazini kuendelea silaha za nyuklia na majaribio yake ya teknolojia ya makombora.
Awali Rais Obama alikutana na viongozi wa Japan na Korea kusini kuweka msimamo wa pamoja juu ya suala la usalama katika rasi hiyo ya Korea.
Pamoja na kwamba nchi ya pili kwa nuklia duniani Urusi haijahudhuria mkutano huo, Rais Obama alifanya mazungumzo na Rais Xi Jinping of China ambapo amesema yeye pamoja na Rais XI wamekubaliana kuondoa nuklia katika eneo la rasi ya Korea na kutekeleza vikwazo vipya vilivyopitishwa na Umoja wa Matiafa kwa lengo la kuipa shinikizo jipya Korea Kaskazini.
Kwa upande wake Rais Xi amesema China inataka kuongeza mawasiliano na kuratibu jambo hilo ambapo nchi zote mbili zimekubaliana kukutana kila mwaka kuzungumzia masuala ya usalama wa nyuklia.
Wamesema pia watafanya kazi kwa pamoja kuzuia malighafi za kutengeneza nuklia na kuratibu juhudi za kuzuia malighafi hizo kuangukia mikononi mwa magaidi.
Hata hivyo kasoro moja katika mkutano huo ni kutokuwepo kwa Rais Vladimir Putin. Urusi na Marekani wanamiliki karibu asilimia 90 ya silaha za nyuklia hivyo Mosco kukataa kuhudhuria mkutano huo unaweza kufanya makubaliano yatakayofikia isiyatekeleze.
Category:
0 comments