PROF JAY AJA UPYAKIMZIKI
Mbunge wa Jimbo la Mikumi na msanii wa muziki, Joseph Haule ‘ Professor Jay’ amesema kuwa yeye ni mwanamuziki na ataendelea kufanya muziki mpaka siku atakapotoweka duniani.
Kupitia instagram, Professor ameandika.
Nimepata salamu nyingi za ‘kunimiss’ kwenye game kutoka kwa mashabiki wangu wengi sana kutoka kona mbalimbali za dunia hii. Ni kweli kabisa kwamba kwa sasa nina majukumu makubwa sana ya kuwatumikia wananchi wenzangu wa jimbo la Mikumi lakini hilo halisababishi mimi kushindwa hata kwa uchache kuendelea kufanya muziki na kuwatendea haki mashabiki wangu wa ukweli walionibeba tangu siku ya kwanza mpaka sasa wanaendelea kuwa pamoja sana na mimi, ikumbukwe mimi ni mwanamuziki na nitaendelea kuwa mwanamuziki mpaka nione kibao kimeandikwa hakuna muziki.Muziki umenilea, muziki umeendesha maisha yangu na familia yangu, muziki ndio ulionipa heshima kubwa sana ulimwenguni, bila muziki leo nisingekuwa mbunge wa Mikumi. Nawaahidi mashabiki wangu wote mliokuwa mnaniuliza mara kwa mara kama nimeacha kufanya muziki kuwa nitaendelea kufanya muziki till i die, maana hiki ni kipaji cha hali ya juu nilichopewa na Mungu kwa makusudi na kwa upendeleo mkubwa na sio kwa bahati mbaya. Nimewasikia na muda sio mrefu nitawatendea haki, ahsanteni sana kwa kuniamini nawapenda sana, huu ni mgodi unaotembea.
Category:
0 comments