MAENDELEO YA ZANZIBAR SASA KUWA CHINI YA RAIS JOHN POMBE MAGUFULI
Rais Magufuli amesema hayo alipokuwa akizungumza na wananchi wa
Zanzibar katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa
Kibandamaiti Mjini Unguja.
Dkt. Magufuli ambaye aliongozana na
Mkewe Janeth Magufuli amesema ili mambo hayo yafanikiwe Wananchi wa
Zanzibar hawana budi kukataa kujihusisha na vitendo vya vurugu na
kuvunja amani na amewaonya watu wanaochochea vitendo hivyo kuacha mara
moja.
Amewataka wananchi wa Zanzibar kujihadhari dhidi ya
wanasiasa ambao wanapandikiza chuki, ubaguzi na fitina, kwani watu hao
wanataka kubomoa misingi mizuri ya umoja, upendo na mshikamano wa Taifa
uliojengwa na waasisi wa Taifa hili.
Rais Magufuli amempongeza
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed
Shein aliyehudhuria mkutano huo, kwa hatua mbalimbali anazozichukua
kuwaletea maendeleo wananchi wa Zanzibar huku akibainisha kuwa tatizo la
maji linalovikabili visiwa vya Zanzibar litakwisha baada ya kutekelezwa
kwa mradi mkubwa wa maji utakaofadhiliwa na Serikali ya India kwa
gharama ya Dola za Marekani Milioni 92, na mradi mwingine
utakaofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa gharama ya
Dola za Marekani Milioni 21.
Aidha, Rais Magufuli amevipongeza
vyombo vya ulinzi na usalama kwa kazi nzuri vinayofanya katika kusimamia
amani visiwani humo huku akivihakikishia kuwa yeye akiwa kiongozi wao
anawaunga mkono.Pamoja na Rais Shein Mkutano huo umehudhuriwa na Mke wa
Rais wa Kwanza wa Zanzibar Mama Fatma Karume, Mawaziri na Viongozi wa
Siasa na wa Dini.
Category:
0 comments