.

.

KOFI ANNAN AZOMEWA MYANMAR

ZePLAN | 01:03:00 | 0 comments

Kofi AnnanWanaharakati wa Kibudha nchini Myanmar wamemzomea na kumkemea katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan.

Bw Annan alizomewa baada ya kuwasili katika jimbo la Rakhine kuchunguza mzozo wa kidini katika eneo hilo.

Mamia ya maelfu ya Waislamu wa jamii ya Rohingya wamefurushwa makao kwenye mashambulio yaliyotekelezwa na Wabudha walio wengi.
Wengi wamenyimwa uraia na kulazimika kuikimbia nchi hiyo.

Mashambulio hayo yamepelekea baadhi ya watu kutilia shaka kujitolea kwa kiongozi wa MyanmarAung San Suu Kyi kutetea haki za kibinadamu.

Bi Suu Kyi alimwita Bw Annan kuchunguza na kupendekeza njia za kupunguza uhasama baina ya jamii zinazoishi eneo hilo.

Bw Annan alihusika kupatanisha pande hasimu wakati wa vita vya baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 nchini Kenya.

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments