SUDAN KUSINI SURA YA UTULIVU NA AMANI NCHINI HUMO YAANZA KUONEKANA
Rais wa Jamhuri ya Sudan Kusini Salva Kiir amemtumia ujumbe Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki akimuarifu kuwa hali ya usalama katika nchi hiyo imeanza kutengemaa.
Mhe. Aggrey Tisa Sabuni amesema Sudan Kusini ipo tayari kushirikiana na nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika masuala mbalimbali yenye manufaa kwa wananchi ikiwemo biashara na uwekezaji na kwamba ni matumaini yake kuwa itapata ushirikiano mzuri.
Kwa upande wake Rais Magufuli ameelezea kufurahishwa kwake na taarifa za kutengemaa kwa hali ya amani nchini humo na kwamba ni matarajio yake kuwa Sudan Kusini itajikita katika maendeleo ya wananchi wake.
Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amepokea ujumbe kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza ulioletwa na Mjumbe Maalum wa Rais huyo Mhe. Aime Laurentine Kanyana.Katika ujumbe huo Rais Nkurunziza amesema hali ya Burundi ni shwari na kwamba wananchi wa Burundi wanaendelea na shughuli zao kama kawaida.
Kwa upande wake Rais Magufuli amesema Tanzania yenye wakimbizi takribani 200,000 wa kutoka Burundi inafurahishwa na taarifa za kuwepo hali ya amani nchini humo.
Category:
0 comments